HabariMilele FmSwahili

Wafanyikazi wa kiwanda cha sukari cha Chemilil waandamana

Wafanyikazi katika kiwanda cha sukari cha Chemilil wameandamana kulalamikia mpango wa kupigwa mnada kiwanda hicho. Wafanyikazi hao pia wanalalamikia kutolipwa mishahara yao huku wakielekezea uagizaji sukari kutoka nje kama chanzo cha masaibu ya kiwanda hicho. Wanaitaka serikali kuingilia kati ili kukimwamua kiwanda hicho.Haya yanajiri siku mbili baada ya wafanyikazi hao kuzuia jaribio la madalali kutwaa umiliki wa kiwanda hicho kinachokabiliwa na madeni.

Show More

Related Articles