HabariMilele FmSwahili

Moto wasababisha hasara katika soko la Korogocho, Nairobi

Wafanyibiashara katika soko la Korogocho wanakadiria hasara baada ya moto mkubwa kuteketeza vibanda zaidi ya 100 usiku wa kuamkia leo. Aidha wametoa wito kwa wahisani kujitokeza kuwasaidia kuendeleza biashara zao.
Kulingana na chifu wa eneo hilo Nyabuto Omache zaidi ya wafanyibiashara 5000 wameathirika kutokana na mkasa huo. Hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa. Aidha amesema kuwa uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha mkasa huo.

Show More

Related Articles