HabariPilipili FmPilipili FM News

Rais Uhuru Atia Saini Mswaada Wa usawazishaji wa fedha za akiba mwaka 2018.

Rais Uhuru Kenyatta ametia saini mswaada wa fedha kuidhinisha matumizi ya shilingi trilioni 1.4 kutoa huduma za umma katika kipindi cha mwaka wa 2018/2019 kuanzia tarehe moja mwezi ujao.

Katika mapendekezo ya bajeti hiyo ya kipindi cha mwaka  wa 2018/2019, shilingi trillion 1.6 zimetengewa Serikali ya Kitaifa, shilingi bilioni 14.8 kutengewa Idara ya Mahakama na shilingi bilioni 36.8 kutengewa bunge.

Kati ya kiasi hicho cha shilingi trilioni 1.6 zilizotengewa serikali ya kitaifa, shilingi bilioni 17.2 zimekusudiwa kutumika kama ruzuku kwa serikali za kaunti.

Katika kiasi cha fedha zilizotengewa serikali za kaunti shilingi  bilioni 9.4 zitatumika kwa kukodisha vifaa vya matibabu, shilingi bilioni 4.3 kwa hospitali za level 5, shilingi bilioni mbili kwa ukarabati wa vyuo vya kiufundi,  shilingi milioni 900 kutumika kwa malipo ya fidia huku shilingi milioni 605 kutumika kwa ujenzi wa makao makuu ya kaunti

Show More

Related Articles