HabariPilipili FmPilipili FM News

Shughli Za Kupaka Majumba Rangi Ya Samawati Na Nyeupe Za Shika Kasi, Mombasa

Serikali ya kaunti ya Mombasa inapania kuendeleza mradi wake wa kupaka rangi majumba ya katikati mwa mji hadi katika miji mingine ya kaunti ya Mombasa.

Katibu wa uchukuzi na miundo msingi Tawfiq Balala amesema awamu ya kwanza ya mradi huo ndio inatarajiwa kukamilika tarehe 30 ya mwezi huu ambapo maeneo ya katikati mwa Mombasa ndio yamelengwa kwanza.

Wakati huo huo amesema makataa ya kutekeleza mpango huo hayataongezwa akisema kufikia kesho wale ambao watakuwa hawajatii agizo hilo watapambana na sheria huku akisema misikiti na makanisa yaliyoko katikati mwa mji hayako kwenye mpango huo wa lazima.

Majengo yote katikati mwa mji yanatakiwa akupakwa rangi ya samawati na nyeupe ambapo wakaazi kwa sasa wako mbioni kutekeleza agizo hilo.

Show More

Related Articles