HabariPilipili FmPilipili FM News

Shughli Za Uvuvi Za Tatizika Katika Kisiwa Cha Mkwiro Huko LungaLunga.

 

Wavuvi  katika kisiwa cha Mkwiro huko Lungalunga  Kwale  wanalalamikia uvuvi haramu unaotekelezwa kwa njia ya bunduki,ulipuaji wa  baruti  na sumu  unaotajwa  kuharibu  bahari na kusambaratisha  biashara  ya samaki  katika kisiwa hicho.

Wakiongozwa na Shamanga Abdallah  anasema uvuvi huo  haramu unatekelezwa  na  wavuvi wa kutoka  kaunti  jirani za kilifi,Mombasa na hata majirani zao kutoka  taifa la Tanzania wanaokuja  kutekeleza shughuli zao za uvuvi katika bahari ya shimoni.

Abdalla akisema  hatua hiyo imewasambaratisha  kimaisha  ikizingatiwa kuwa wanategemea  biashara  ya  uvuvi  kujikimu kimaisha  wakiitaka serikali ya kitaifa na ile ya kaunti  kueka mikakati  kabambe   ya  kuhakikisha kuwa   uvuvi  haramu   unakomeshwa katika  eneo hilo  .

Haya yanajiri huku wavuvi hao wakilalamikia  kuvua samaki wachache zaidi  wa hadi  kilo 2 kila siku kinyume na ilivyokua hapo awali ambapo wanasema kuwa walikua wakivua  hadi kilo 500 kwa siku

Show More

Related Articles