HabariMilele FmSwahili

Zaidi ya magunia 600 ya makaa yanaswa kaunti ya Kitui

Zaidi ya magunia 600 ya makaa yamenaswa na polisi kwa ushirikiano na maafisa wa ukaguzi wa serikali ya kaunti ya Kitui,katika gari lililonuia kuyasafirisha hadi hapa jijini Nairobi. Hata hivyo washukiwa waliokuwa kwenye gari hilo wamefanikiwa kukwepa kukamatwa. kamanada wa polisi kaunti ya Kitui Anthony Kamitu amesema wamepata makaa hayo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa umma.

Kamitu awaonya wakazi dhidi ya kujihusika katika biashara iliyopigwa marufuku ya makaa.

Show More

Related Articles