HabariMilele FmSwahili

Waziri Matiangi afika mbele ya kamati ya bunge kuhusu kilimo na biashara

Waziri wa usalama wa taifa Dr.Fred Matiang sasa anasema sukari ilionaswa nchini iliingizwa kwa kutofuata sheria hitajika. Hata hivyo Matiang’ amabye anafika mbele ya kamati ya pamoja kuhusu biashara na kilimo,anasisitiza baadhi ya sukari hiyo sio salama. Anasema kufikia sasa gunia milioni 1.4 za sukari zimenaswa huku watu 72 wakikamatwa na uchunguzi unaendelea.

Anasema nyingi ya sukari ilio na utata iliingia nchini kupitia mipaka ya Kenya Isiolo na usalama wa kutosha na kukana madai ilipitia bandari ya Mombasa.

Show More

Related Articles