HabariMilele FmSwahili

Watu wasiopungua 15 wafariki katika mkasa wa moto katika soko la Gikomba

Watu wasiopungua 15 wafariki kufuatia mkasa wa moto katika soko la Gikomba hapa Nairobi. Kulingana na mshirikishi wa kanda ya Nairobi Kangethe Thuku watu wengine 70 wamejeruhiwa. Amesema kuwa maafisa wa uokozi wanajitahidi kuondoa miili ya wati 9 kutoka majengo ya makazi yaliyoteketea. Majeruhi wa mkasa huo wanapokea matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta.

Kangethe pia amesema uchunzi unaendelea kubaini chanzo cha mkasa huo. Kadhalika kituo maalum cha kupokea maelezo kimebuniwa kuwahudumia jamaa za waathrika

Baadhi ya walioshuhudia mkasa huo wanadai kuwa ulichangiwa na hitilaf ya za nguvu za umeme

Show More

Related Articles