HabariSwahili

Mchuuzi aliyedhaniwa askari kwa kumuuzia Ruto mahindi azungumza

Mchuuzi wa mahindi ya kuchoma kutoka Kiambu ambaye amesifika mitandaoni kwa kupata nafasi ya kumhudumia naibu rais William Ruto na kwa kumuuzia mahindi amejitokeza na kukana madai kwamba yeye ni mmoja wa walinzi wa naibu rais William Ruto aliyeigiza na kujifanya muuza mahindi.

Naibu rais William Ruto alipokuwa kwenye ziara ya kisiasa eneo la Githunguri kaunti ya Kiambu wiki iliyopita alisimama eneo moja kando ya barabara na kujiburudisha na lishe ya mahindi ya kuchoma, hata hivyo, kitendo hicho kilizua cheche mitandaoni wengi wakisema kitendo hicho kilipangwa mapema na kuigizwa.

Dennis Matara alimpata muuzaji huyo wa mahindi choma na kukuandalia taarifa hii.

Show More

Related Articles