HabariMilele FmSwahili

Zaidi ya lita 2500 za Ethanol zilizoingizwa nchini kimagendo zanaswa Migori

Polisi katika eneo la Nyatike kaunti ya Migori wamenasa lita zaidi ya 2500 za kemikali ya Ethanol yenye dhamani ya shilingi milioni 20 inayodaiwa kuingizwa nchini kimagendo kutoka Tananzia. Kamishna wa kaunti ya Migori Joseph Rotich amedhibitisha kuwa kemikali hiyo iliyokuwa katika mapipa 81 imepatikana baada ya maafisa wa ushuru wa kaunti hiyo kusimamisha lori lililokuwa liisarifisha kwenye bara bara ya Migori-Sori. Hata hivyo dereva pamoja na washukiwa wengine waliokuwa kwenye lori walitoroka kabla ya polisi kuwanasa. Polisi wanachunguza ilikotoka kemikali hiyo na ilikokuwa inaelekezwa.

Show More

Related Articles