HabariMilele FmSwahili

Bwala la Patel lililovunja kingo zake halikuwa na leseni ya NEEMA

Bwawa la Patel huko Solai kaunti ya Nakuru lililovunja kingo zake na kuwauwa watu 46 halina leseni ya mamlaka ya NEEMA. Kamati ya seneti inayochunguza mkasa huo imeelezwa kuwa,bwawa hilo lilichimbwa kabla ya NEEMA kubuniwa japo NEEMA ilikua imeanza kulikagua kabla ya mkasa huo. Hata hivyo NEEMA imeiambia kamati hiyo yake seneta Mutula Junior, mabwawa mengine matano yalio eneo hilo yamekaguliwa na kuidhinishwa kuwa salama.

Show More

Related Articles