HabariPilipili FmPilipili FM News

Walemavu Wamtaka Rais Uhuru Kuchagua Bodi Ya Kusimamia Masilahi Yao.

Msemaji wa walemavu nchini Joseph Nganga Kuria amemtaka rais Uhuru Kenyatta pamoja na naibu wake William Ruto kuchagua bodi ya kusimamia maswala ya walemavu ili jamii inayoishi na ulemavu wapate huduma zao za kimsingi.

Kulingana na Nganga mwaka wa kifedha uliopita serikali ya kitaifa ilitenga takriban shillingi billion 1.2 fedha  za kushughulikia maswala ya walemavu lakini kutokana na kutokuwepo kwa bodi hiyo ya kusimamia walemavu fedha hizo hadi kufikia sasa bado hazijatumika.

Nganga ambaye pia ni afisa mkuu wa idara ya vijana na walemavu katika kaunti ya Lamu amesema ukosefu wa bodi hiyo umepelekea walemavu wengi nchini kukumbwa na changamoto ikiwemo kukosa elimu ,vifaa wanavyotumia kutembelea sawia na mafuta ya kujipaka ya walemavu wa ngozi.

Show More

Related Articles