HabariPilipili FmPilipili FM News

Kaunti Ya Mombasa Yatoa Makataa.

Serikali ya kaunti ya Mombasa imetoa makataa ya hadi mwisho wa mwezi huu ya kupakwa rangi ya samawati na nyeupe majengo yaliyoko katikati mwa mji wa Mombasa.

Hii ni baada ya serikali ya kaunti ya Mombasa kutoa mwelekezo wa majumba hayo kupakwa rangi ili kuboresha mazingira ya mji wa Mombasa.

Akizungumza na meza yetu ya habari katibu wa uchukuzi Tawfiq Balala amesema watawafkisha  mahakamani wale wote watakaokaidi amri hiyo.

Kwa upande mwingine katibu wa kaunti Francis Thoya amesema watu wote wanatakiwa kukubaliana na kanuni hiyo hata yale mashirika yenye kutumia rangi tofauti akilipigia mfano shirika la safaricom.

Aidha amawetaka wamiliki wote wenye kuendesha biashara katikati ya mji kuweka mataa meupe katika maeneo wanayofanyia biashara zao.

Show More

Related Articles