HabariPilipili FmPilipili FM News

Vita Dhidi Ya Mihadarati Kuendelea Mombasa.

Takribani vijana elfu 18 wamejiingiza kwenye uraibu wa kutumia Mogokaa kaunti ya Mombasa.
Kulingana na mwanaharakati mmoja wa madawa ya kulevya kwenye kaunti hiyo vijana wengi wamejiingiza kwenye uraibu huo huku akitaja kuwa ni janga ambalo limewathiri vijana wengi kwa kuwasababishia maradhi ya akili.
Aidha kamishna wa kaunt ya Mombasa Evans Achoki amesema vita dhidi ya mihadarati vinaendelea huku akiutaja mtaa wa Magodoroni eneo bunge la Kisauni kama ulioathirika zaidi na utumizi wa mihadarati.
Pia amesema wanaendesha operasheni kwenye maduka ya kuuza dawa ili kukomesha matumizi ya vibugizi.

Show More

Related Articles