HabariPilipili FmPilipili FM News

Wasimamizi Wa Shirika La KEBS Kufikishwa Mahakamani Leo.

Maneja mkurugenzi wa shirika la ubora wa bidhaa nchini KEBS Charles Ongwae pamoja na maafisa wengine wanne wakuu wa shirika hilo watafikishwa mahamani  leo kujibu mashitaka kuhusiana na sakata ya uagizaji bidhaa ghushi.

Ongwae pamoja na mkuu wa kitengo cha ubora Eric Chesire Kiptoo, meneja wa ukaguzi katika bandari ya kilindini Peter Kinyanjui maneja wa KEBS kanda ya Pwani Martin muswanya nyakiamo na afisa wa afya katika bandari ya kilindini pole mwangeni pia watajibu mashitaka ya jaribio la mauaji.

Mkurugenzi wa mashitaka ya umma Noordin Haji pia ameagiza kushitakiwa kwa kampuni ya OCP Kenya kwa kuagiza kiligramu milioni 5.8 za mbolea hiyo kutoka nchini Morocco kwa njia ya ulaghai madai ambayo kampuni hiyo imekanusha.

Show More

Related Articles