HabariMilele FmSwahili

Rais awataka magavana kuunga mkono juhudi za serikali kumaliza ufisadi

Rais Uhuru Kenyatta amewataka magavana kuunga mkono juhudi za serikali kumaliza ufisadi nchini. Akizungumza alipokutana na magavana katika ikulu ya Nairobi rais Kenyatta amesisitiza kuhusu tishio la ufisadi kwa ustawi wa taifa. Amewaonya dhidi ya kushiriki katika uporaji wa pesa za umma. Aidha rais Kenyatta amewahimiza magavana kushirikiana na serikali yake katika utekelezaji agenda nne kuu za utawala wake ili kuafikia maendeleo ya kitaifa. Pia amesema serikali serikali itaendelea kushirikiana na magavana katika kufanikisha maendeleo mashinani.

Show More

Related Articles