HabariMilele FmSwahili

Raila akutana na kushauriana na balozi wa Marekani nchini Robert Godec

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga leo amekutana na kushauriana na balozi wa Marekeni nchini Robert Godec. Mkutano huu umeandaliwa katika afisi za ODM Capitol Hill hapa Nairobi wawili hao wakijadiliana masuala ya kudumisha amani nchini South Sudan. Raila alikwua miongoni mwa walioongoza mazungumo ya kuwaleta pamoja viongozi waliohasimiana katika taifa hilo. Pia wamejadili jinsi ya kuleta umoja nchini na ziara ya aliyekuwa rais wa marekani Barrack Obama humu nchini.

Show More

Related Articles