HabariMilele FmSwahili

Mahakama yaruhusu kuachiliwa huru kwa Lilian Omollo na Richard Ndubai

Katibu wa vijana aliyesimamishwa Lilian Omolo na mkurugenzi wa NYS Richard Ndubai wako huru. Hii ni baad ya jaji wa mahakama kuu Lawerence Mugambi kutupilai mbali ombi la mkurugenzi wa mashtaka ya umma kuendelea kuwazuilia kuchunguza pesa na stakabadhi zingine za washukiwa wa sakata hiyo. Akitoa uamuzi wake anasema iwapo mahakama itaruhusu ombi hilo huenda ikaenda kinyume na maamuzi yake binfasi ya kuwaachilwia kwa dhamana. Pia anasema haitakwua sawa kuwanyima dhamana kwani wameafikia vigezo vyote vilivyowekwa na mahakama kulipia dhamana hiyo. Aidha amesema uamuzi huo utakuwa unakwenda kinyume na mwongozoa wa mahakama na haki za washukiwa hao.

Amemtaka mkurugenzi wa mashtaka ya umma kutafuta mbinu mbadala ya kuhakiki iwapo wadhamini wao na pesa walizowasilishwa kuachiliwa ni kait ya zile wanazodaiwa kupora kutoka NYS.

Show More

Related Articles