HabariPilipili FmPilipili FM News

Zaidi Ya Kaunti 23 Zimeathirika Na Ukosefu Wa Sodo Kwa Wasichana Wa Shule.

Asilimia 75 ya wasichana wa shule kote nchini hukosa kuhudhuria  masomo yao kikamilifu kila mwezi, kutokana  na ukosefu  wa sodo wakati  wa hedhi.

Hayo ni kulingana na afisaa  wa  afya ya umma kutoka wizara ya afya nchini  Janet Mule ambaye anasema zaidi ya kaunti  23 zimeathirika  na tatizo hilo, zikiongozwa na  kaunti za  baringo ,pokot magharibi na turkana.

Kwa upande wake Christine Mwaka Mvurya aliye mkewe gavana wa kwale  na mwenzake wa makueni Nancy Kivutha  wameeleza  kuwa  wake wa magavana  humu nchini  tayari wameanzisha mradi wa miaka 3, wa kusambaza sodo wakilenga jumla ya wasichana milioni 1 na zaidi ikiwa ni katika juhudi za kuimarisha elimu ya mtoto wa kike

Show More

Related Articles