HabariMilele FmSwahili

Wakazi wanaoishi kando ya reli Kibera walalamikia ubomozi wa nyumba zao

Wakazi wanaoishi kando ya reli mtaani Kibera wameachwa bila makao kufuatia shughuli ya ubomozi wa majengo yao. Kadhalika taharuki imetanda katika mtaa huo polisi wakiwarushia vitoa wenyeji hao waliojaribu kuzuia ubomozi huo. Ubomozi huo unaoendeshwa na taasisi mbali mbali za serikali pia umehusishwa kukatizwa huduma za umeme unaodaiwa kuunganishwa kinyume na sheria. Wakazi wameshutumu hatua hiyo wakidai hawakujuzwa kuihusu.

Show More

Related Articles