HabariMilele FmSwahili

Zaidi ya mashine 80 za mchezo wa kamari zateketezwa Kakamega

Zaidi ya mashine 80 za mchezo wa kamari kaunti ya Kakamega zimeteketezwa moto. Ni kufuatia agizo la waziri wa usalama wa ndani Dr Fred Matiangi ambaye ameamrisha mashine hizo kuteketezwa kutokana na athari yake kwa vijana nchini. Kamishna wa Kakamega Abdirisack Jaldesa aliyeongoza maafisa wengine wa usalama kwa shughuli hiyo ameahidi kuziteketeza mashine zote kaunti yake akiwataka wamiliki kusita kuzificha

Show More

Related Articles