HabariMilele FmSwahili

Polisi wanasa malori 9 yaliyobeba sukari inayokisiwa kuwa na sumu Rongo

Polisi huko Rongo kaunti ya Migori wanazuilia malori 9 yaliobeba sukari inayokisiwa kuwa na sumu. Inadaiwa sukari hiyo ilikuwa ikisafirishwa kwa muuzaji mmoja kaunti ya Homabay. Katika eneo la Chuka kaunti ya Tharaka Nithi polisi wanazuilia magunia 800 ya sukari inayodaiwa kuwa na madini ya shaba yaani copper na zabeki yaani mercury. Yanajiri hayo huku kiongozi wa wengi bungeni Adan Dualle akitarajiwa leo kuweka bayana majina ya wanaohusika na biashara ya sukari ya sumu. Dualle anasema ni sharti asasi za usalama nchini kuwaadhibu wahusika wa biashara hiyo ili kuokoa maisha ya wakenya.

Show More

Related Articles