HabariMilele FmSwahili

Hakimu Douglas Ogoti kutoa mwelekeo kuhusu kesi ya sakata ya NYS leo

Hakimu wa mahakama ya ufisadi Douglas Ogoti anatarjiwa leo kutoa mwelekeo kuhusiana na kesi za washukiwa 43 wa sakata ya ufisadi katika shirika la huduma kwa vijana NYS. Hii ni baad ya mahakama hapo jana kuwaachiliwa kwa dhamana wote hao. Hakimu Ogoti ataamua sasa tarehe ya kuendelea kuskizwa kesi dhidi ya wote hao ambao tayari wamekana kushiriki wizi huo. Wanashtakiwa miongoni mwa makosa utumizi mbaya wa mamlaka na kuvunja sheria za ununuzi.

Show More

Related Articles