HabariMilele FmSwahili

Kesi mbili za kupinga mpango wa serikali kuwaajiri madaktari kutoka Cuba zatupiliwa mbali

Mahakama kuu imetupilia mbali kesi mbili za kupinga mpango wa serikali kuwaajiri madaktari kutoka Cuba. Kwenye uamuzi wake,jaji Onesmus Makau amesema walalamishi hawakudhibitisha madai kwamba haki za madaktari wa kenya zilikiukwa katika kuwaajiri madaktari hao kutoka Cuba. Hata hivyo,jaji Makau ameikosoa wizara ya afya kwa kutoshauriana na muungano wa madaktari nchini KMPDU katika mpango huo ili kutoa maoni yao. Uamuzi huo sasa unatoa nafasi kwa madaktari hao 100 ambao tayari wamewasili nchini kutumwa kaunti tofauti nchini kuanza kuhudumu kwa kandarasi ya miaka miwili.

Show More

Related Articles