HabariMilele FmSwahili

Washukiwa wa sakata ya NYS waachiliwa kwa bondi ya milioni 5 kila mmoja

Ni afueni kwa washukiwa wa sakata ya NYS baada ya mahakama kuu kuwaachilia kwa dhamana. Jaji Hedwig Ongundi amewaagiza katibu wa masuala ya vijana Lillian Omollo na mkurugenzi wa shirika la NYS Richard Ndubai na washukiwa wengine kuachiliwa kwa bondi ya shilingi milioni 5 kila mmoja. Aidha washukiwa watahitajika kuripoti kwa afisi za idara ya ujasusi DCI, kuhudhuria kesi zao kila watakapohitajika na pia kuwasiilisha vyeti vyao vya usafiri kwa mahakama.

Show More

Related Articles