BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Msanii Wa Nyimbo Za Rap Kutoka Marekani XXXTentacion Auawa.

Mwanamuziki wa nyimbo za rap Marekani XXXTentacion, ambaye alipata umaarufu kwa haraka kupitia albamu zake mbili ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa na miaka 20.

Alikuwa anaondoka kwenye duka la kuuza pikipiki kusini mwa Florida Jumatatu pale mtu mwenye bunduki alipomfyatulia risasi.

Polisi katika tarafa ya Broward wanasema XXXTentacion, ambaye jina lake Jahseh Onfroy, alikimbizwa hospitalini lakini akathibitishwa kufariki.

Show More

Related Articles