HabariPilipili FmPilipili FM News

Wafungwa Wawili Watoroka Gerezani Malindi.

Maafisa wa magereza wanaendesha uchunguzi kubaini jinsi  wafungwa wawili walifanikiwa kutoroka  katika gereza la Malindi kaunti ya kilifi.

Mkuu wa idara ya magereza kanda ya Pwani Joseph Mutevesi amethibitisha kutoroka kwa wafungwa hao,akisema walitoweka wakiwa katika shughuli zao za gareza ,  chini ya usimamizi wa maafisa wa gereza hilo.

Mutevesi anasema haijabainika nini hasa kilisababisha wafungwa hao Jacob Tembo Deche na Karisa Kahindi wote wakazi wa kilfi kutoroka , akiongeza kuwa tayari  idara ya upelelezi imeanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo.

Afisa huyo amewaomba wanachi kupiga ripoti kwa polisi endapo watapata taarifa zozote kuhusu wawili hao.

Show More

Related Articles