HabariMilele FmSwahili

Idara ya usalama wa taifa yadaiwa kununua helikopta 4 kwa shilingi bilioni 4.6 bila idhini ya bunge

Wizara ya usalama wa taifa inadaiwa kununua helikopta nne kwa shilingi bilioni 4.6 bila idhini ya bunge. Ndege hizo zitatumiwa na maafisa wa polisi wa kitengo cha anga na zinatarajiwa kuwasili nchini hivi leo kutoka Italia na Canada. Hata hivyo mamlaka ya kusimamia masuala ya ndege nchini inatishia kufutilia mbali leseni ya idara hiyo ya polisi kwa kukosa kufuatia maagizo yake ikiwemo kuwapa bima marubani na ndege wanazotumia. Awali wakizungumza baada ya kuzuru makao makuu ya kitengo cha ndege cha maafisa wa polisi uwanja wa Wilson, wabunge wa kamati ya usalama wameelezea kushangazwa na jinsi ndege hizo zilinunuliwa bila idhini ya bunge. Hata hivyo katibu katika wizara ya usalama wa taifa alilaumiwa kutokana na hilo. Kupata taarifa hii kwa kina jipatie gazeti lako la people daily.

Show More

Related Articles