People Daily

Seneta Wa Migori Ben Oluoch Afariki Dunia .

 

Kulingana na jamaa za familia seneta Oluoch alifariki katika hospitali ya MP-Shah wakati akiendelea kupokea matibabu.

Seneta huyo ambaye pia alikuwa mtangazaji wa Radio idhaa ya Ramogi, inaarifiwa  amekuwa akiugua saratani ya koo kwa mda.

Millie Odhiambo na David Osiani ni miongoni mwa viongozi waliofika hospitalini kuthibitisha kifo cha seneta wa Migori Ben Oluoch.

Kulingana na jamaa za familia mwili wa marehemu unahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Lee Jijini Nairobi wakati mipango ya mazishi ikiendelea.

Show More

Related Articles