HabariSwahili

Wenyeji Karatina wahama makaazi yao ya kihafari kwa kuhofia maisha

Wenye makaazi ya kifahari karibu na mji wa Karatina, kaunti ya Nyeri wamelazimika kuhama na kuishi katika baadhi ya hoteli mjini humo, baada ya kuhangaishwa na kushambuliwa mara kadhaa na majambazi, wengi ambao ni vijana barobaro waliojihami kwa bunduki.

Wahalifu hao wenye sarakasi nyingi wanasemekana hata kuwa na wakati wa kula chakula cha waathiriwa na hata kuwa na muda wa kupika chakula kingine, wanapotekeleza maovu yao usiku.

Mwanahabari wetu Grace Kuria alizuru eneo bunge la mathira na kushuhudia kwa nini sehemu hiyo imekuwa himaya ya majambazi.

Show More

Related Articles