HabariMilele FmSwahili

Shehena 89 za bidhaa ghusi zazuiliwa katika mabohari ya serikali Embakasi, Nairobi

Serikali inazuilia shehena 89 katika mabohari yake eneo la Embakasi Nairobi baada ya kupatikana bidhaa zote zilizoko katika shehena hizo ni gushi. Katibu katika wizara ya utumishi wa umma Wanyama Musiambo anasema bidhaa hizo za ghamara ya shilingi bilioni 1.2 zote zitaharibiwa. Miongon mwa bidhaa zilizopatikana katika shehena hizo ni nguo za ndani, nyaya za stima, mafuta ya kukula miongoni mwa bidhaa zingine.

Wakati huo maelfu ya magunia ya sukari bandia yamenaswa kaunti ya Meru. Uongozi wa usalama Meru unasema washukiwa wametiwa mbaroni baada ya kupatikana wakipakia sukari hiyo kuwauzia wenyeji

Show More

Related Articles