HabariMilele FmSwahili

Matiang’i atoa makataa kwa mashine zote za kamare nchini kuharibiwa

Waziri wa usalama wa ndani Dr Fred Matiangi ametoa makataa ya hadi mwishoni mwa mwezi huu kuharibu mashine zote za mchezo wa kamare nchini. Matiangi anasema machifu na polisi watatakiwa kuwajibika katika zoezi hilo ambalo limekuwa likielendeshwa kote nchini. Akizungumza baada ya kushuhudia kuharibiwa kwa mashine hizo eneo la Dagoreti Corner hapa Nairobi, Matiangi ameahidi kuitokomeza biashara hiyo

Anasema iwapo kunao maafisa serikali watapatikana wamehusika na biashara hiyo wataachishwa kazi mara moja

Show More

Related Articles