HabariMilele FmSwahili

Vikao vya kupokea ushahidi wa umma kuhusu mauaji ya mtoto Pendo vyaendelea Kisumu

Vikao vya kupokea ushahidi wa umma kuhusu mauaji ya mtoto Pendo vinaendelea wakati huu mjini Kisumu. Maafisa wakuu wa usalama kaunti ya Kisumu wanatarajiwa kufika mbele ya hakimu Beryl Ommollo kuelezea wanachofahamu. Hii ni baada ya vikao kuahirishwa wiki iliyopita baada ya kamanda wa polisi wa Kisumu Central Benjamin Kosgei kusema hakujuzwa kuhusiana na mpangilio wa utendakazi wa maafisa wa usalama walioshika Doria wakati na baada ya uchaguzi mjini humo.

Show More

Related Articles