HabariPilipili FmPilipili FM News

Raila Akanusha Madai Kwamba ODM Imeandaa Mkutano Kujadili Changamoto Za Chama Hicho.

Chama cha ODM kinaandaa mkutano wake wa kitaifa hapa mombasa kutafakari mikakati ya kukiimarisha chama hicho.

Raila Odinga aliye kinara wa chama hicho anasema lengo kuu la mkutano huo ni kujadili ajenda za chama, na kwamba mkutano huo unahusisha wajumbe pamoja na maafisa wengine wa chama hicho kutoka maeneo yote nchini.

Kauli sawa na hiyo imetolewa na gavana wa mombasa Hassan Ali Joho ambaye ndiye mwenyeji wa mkutano huo. Wengine wanaohudhuria mkutano huo ni pamoja na gavana wa kilifi Amason Jeffa Kingi miongoni mwa wengine.

Awali kumekuwa na madai kwamba mkutano huo ulilenga kujadili changamoto za chama ikiwemo kuwaadhibu baadhi ya viongozi, wanaoonekana kuchukua mkondo mpya kuhusiana siasa  za mwaka wa 2022.

Show More

Related Articles