HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanaoenda Baharini Kuogelea Waombwa Kuwa Makini Zaidi.

Kikosi cha uokoaji katika bahari hindi mjini Kilifi kimetoa tahadhari kwa wavuvi na  wananchi ambao wanaenda baharini kuogelea kuwa makini.

Maafisa wa Kikosi hicho wanasema kwa sasa kunashuhudiwa mawimbi makali baharini ambayo ni hatari kwa usalama wa wananchi wanaotembelea maeneo hayo.

Nahodha Shallo Issa ambaye ni mwenyekiti wa kikosi hicho amesema kuna maeneo ambayo wameyaorodhesha kuwa hatari zaidi wakati huu ikiwemo vidazini,members na  Roka Maweni pamoja na Uyombo.

Show More

Related Articles