HabariPilipili FmPilipili FM News

Maafisa Wa Polisi Wauawa Katika Shambulizi La Kigaidi.

Maafisa 8 wa polisi wamethibitishwa kuuawa katika uvamizi ulitekelezwa na kundi la Alshabab kaunti ya Waajir.

Kulingana na idara ya polisi eneo hilo, kati ya nane hao watano ni kutoka kitengo cha polisi ya utawala huku wengine watatu wakiwa sehemu ya polisi jamii ya kaunti hiyo.

Mshirikishi wa serikali kaskazini mashariki mwa nchi Muhamud Saleh amesema maafisa hao walifariki baada ya gari lao walimokuwa wakisafiria kukanyaga kilipuzi katika eneo la Bojigaras.

Kulingana naye hicho ni kisa cha tatu cha uvamizi kutekelezwa eneo hilo tangu mwaka huu wa 2018 uanze.

Show More

Related Articles