HabariMilele FmSwahili

Waislamu waadhimisha siku kuu ya Idd-Ul-Fitr

Waislamu waadhimisha siku kuu ya Idd-Ul-Fitr

Kukithiri kwa ufisadi nchini na ripoti za ubakaji kwa wanafunzi ni baadhi ya mambo yaliotawala maombi maalum ya kuadhimisha siku kuu ya Idd-Ul-Fitr. Viongozi wa kidini na kisiasa waliohudhuria maombi hayo sehemu tofauti nchini wametaka masuala hayo kupewa kipau mbele wakionya hatari ya taifa kukosa mwelekeo iwapo hayatakomeshwa. Kadhi mkuu nchini Sheikh Ahmed Muhdhar na mtangulizi wake Sheikh Hammad Kassim ambao waliongoza maombi hayo katika uwanja wa shule ya msingi ya Ronald Ngala mjini Mombasa wamewasihi wakenya kuzingatia utangamano na umoja baina yao.

Naye Gavana Ali Hassan Joho aliyewaongoza viongozi kadhaa wa kisiasa kushiriki maombi hayo amesisitiza haja ya wakenya kuungana kuhakikisha taifa linafaikia ajenda yake kimaendeleo.

Kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale aliyeshiriki maombi hayo katika shule ya Sir Ali Muslim hapa Nairobi ametaka wahusika wa sakata za ufisadi kukabiliwa kibinafsi bila kuhusisha jamii zao.

Show More

Related Articles