HabariPilipili FmPilipili FM News

Joho Aapa Kushirikiana Na Rais Uhuru Ili Kufanikisha Ajenda Nne Za Serikali.

Gavana wa Mombasa Hasan Ali Joho ameapa  kushirikiana na Rais Uhuru Kenyatta ili kufanikisha ajenda nne za serikali kwa manufaa ya wananchi.

Joho amesema sasa tofauti yake na rais Kenyatta imekwisha  akisema atafanya kazi na serikali ili kumaliza nyufa za kisiasa na mgawanyiko  humu nchini.

Naye rais Kenyatta amekemea vikali siasa za chuki akisema wakenya wanasubiri maendeleo mashinani hivyo kuwataka viongozi kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya wakenya.

Wawili hawa wameongea huku miritini wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya kwanza ya barabara ya dongo kundu.

Show More

Related Articles