HabariMilele FmSwahili

Shinikizo zazidi kutolewa kwa serikali kuwaadhibu wanaoagiza sukari bandia nchini

Shinikizo zinazidi kutolewa kwa serikali kuwakamata na kuwaadhibu matapeli wanaoingiza sukari bandia iliyo na sumu  nchini ya hivi punde ikiwa ilionaswa katika kiwanda cha Rai Paper huko Webuye kaunti ya Bungoma. Akizungumza katika ufunguzi  wa maonyesho ya kilimo mjini Kakamega,mbunge wa Lurambi Titus Khamala amesema sukari hiyo inayotoka mataifa ya nje huingizwa nchini na baadhi ya wanasiasa na viongozi wakuu serikalini jambo ambalo limechangia kampuni za kutengeneza sukari  nchini kufilisika. Amesema sukari hiyo gushi imepelekea kufungwa viwanda vya sukari nchini akisema kuna haja ya serikali kubadili mbinu za kuwakabili matapeli ili kuokoa maisha ya wakenya.

Show More

Related Articles