HabariPilipili FmPilipili FM News

Waumini Wa Dini Ya Kiisilamu Wajumuika Pamoja Katika Swala La Eid.

Huku waumini wa dini ya kiisilamu wakiadhimisha siku kuu ya Eid-Ul Fitir katika maeneo mbali mbali ulimwenguni, jumbe za amani na upendo zimesheheni kutoka kwa viongozi wakati wa swalaa ya Eid humu nchini.

Gavana wa mombasa Hassan Ali Joho amewashukuru waisilamu na wakazi wa mombasa kwa ujumla, kwa kuzingatia ushirikiano na utulivu wakati wote wa msimu wa ramadhani.

Kauli sawia na hiyo imetolewa na viongozi mbali mbali akiwemo mbunge wa mvita Abdulswamad Sharrif Nassir pamoja na cHief Kadhi mkuu Ahmed Sharrif Mudhar ambaye amehimiza zaidi amani , upendo na umoja wa wananchi na hata viongozi.

Hapa mombasa waumini wa dini ya kiisilamu, wamejumuika pamoja kwa swalaa ya Eid, katika uwanja wa shule ya msingi ya Ronald Ngala na pia misikiti mbalimbali.

Sherehe za Eid huandaliwa kote ulimwenguni kila mwaka wakati wa kukamilika kwa mwezi mtukufu wa ramadhani.

Show More

Related Articles