HabariMilele FmSwahili

COTU yapinga pendekezo la kuwa na mwakilishi mmoja katika bima ya NHIF

Muungano wa wafanyikazi nchini COTU umepinga pendekezo la kuwa na mwakilishi mmoja pekee katika bodi ya bima ya afya nchini NHIF. Akifika mbele ya kamati ya bunge kuhusu afya, katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli amekosoa marekebisho yanayopendekezwa kwenye sheria kuhusu NHIF ili kutekeleza mabadiliko hayo. Atwoli anataka COTU kupewa nafasi nne kati ya kumi na mbili za walio kwneye bodi hiyo.

Kwenye marekebisho yaliyopendekezwa kwenye sheria hiyo, wawakilishi wa COTU, wale wa walimu, na muungano wa waajiri watapunguzwa na nafasi zao ambazo ni tano, kujazwa na wawakilishi watakaoteuliwa na waziri wa afya.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.