HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakuu Wa Vitengo Vya Ununuzi Wapewa Makataa Ya Wiki Moja.

Wakuu wa vitengo vya ununuzi pamoja na wahasibu katika mashirika ya umma wana mda wa hadi ijumaa wiki ijayo kuwasilisha stakabadhi zao pamoja na maelezo muhimu ili kurahsisha mchakato wa kuwakagua upya.

Msemaji wa serikali Erick Kiraithe anasema stakabadhi hizo zinapaswa kuwasilishwa katika jumba la Harambee jijini Nairobi, kabla ya saa kumi na moja siku hiyo.

Kiraithe, amesema mchakato wa kuwakagua maafisa hao utafanyika kwa njia ya haki na uwazi kulingana na katiba.

Hii ni baada ya mahakama ya leba nchini kufutilia mbali agizo la mahakama, lililokuwa limetolewa kupinga mchakato huo.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.