HabariMilele FmSwahili

Kesi ya kupinga ushindi wa gavana Anyang’ Nyong’o yatupiliwa mbali

Gavana wa Kisumu Anyang’ Nyong’o amepata afueni baada ya mahakama ya rufaa mjini Kisumu kutupilia mbali kesi ya kupinga kuchaguliwa kwake. Majaji Fatuma Sichale, Otieno Odek na Philip Waki wameamua kuwa kesi hiyo iliyowasilishwa na aliyekuwa gavana Jack Ranguma haina msingi. Majaji hao wamesema Ranguma hakuwasilisha ushahidi kudhubitisha lalama zake. Kadhalika wameamua kuwa dosari zilizoshuhudiwa kwenye fomu 34 a na 34b na kutojumuishwa kwa matokeo ya kura katika vituo vitano vya uchaguzi hakukuathiri kivyovyote matokeo ya uchaguzi huo. Wakili wa Nyong’o James Orengo amepongeza uamuzi huo akiutaja kuwa wa haki.

Naye Gavana Nyong’o amesema uamuzi huo unatoa fursa kwake kutimiza miradi ya maendeleo alizowaahidi wakazi wa Kisumu.

Show More

Related Articles