HabariMilele FmSwahili

Kaunti ya Nairobi kunufaika na mpango wa serikali kujenga makaazi ya bei nafuu

Kaunti ya Nairobi itakuwa ya kwanza kunufaika na mpango wa serikali kujenga makaazi ya bei nafuu chini ya ajenda nnne kuu za utawala wa rais Uhuru Kenyatta. Naibu rais William Ruto ametangaza kuwa serikali kuu itaendelea kuunga mkono juhudi za gavana wa Nairobi Mike Sonko kulisafisha jiji la Nairobi na Kuboresha hadhi yake. Akizungumza katika iftar iliyoandaliwa na gavana Sonko kwenye ukumbi wa City naibu rais kadhalika ametoa changamoto kwa wanasiasa nchini kuhubiri amani na mshikamano hasaa kufuatia mwafaka baina ya serikali na upinzani.
Kwa upande wake gavana Sonko ameapa kushirikiana na viongozi wengine ili kuimarisha utendakazi wa serikali yake.
Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka aliyehudhuria hafla hiyo amempongeza amri ya rais Uhuru Kenyatta kwa wizara zote na mashirika ya serikali kuchapisha maelezo ya zabuni zinazotolewa kuanzia Julai Mosi mwaka huu ili kukaguliwa na umma. Ameelezea imani hatua hiyo itafanikisha vita dhidi ya ufisadi nchini.

Show More

Related Articles