HabariMilele FmSwahili

Kesi ya kuhalalishwa kwa ukeketaji wa kina dada kuamuliwa leo

Mahakama kuu ya Machakos leo itatoa uamuzi kuhusiajna kesi ambapo daktari Tatu Kamau anataka ukeketaji wa akina dada kuhalalishwe kisheria. Jaji David Kemei anatarajiwa kuamua iwapo sheria zinazohalalisha ukeketaji zinakwenda kinyuma na katiba. Pia ataamua iwapo bodi ya kupinga ukeketaji itavunjwa. Katiia kesi hiyo dkt Kamau amekuwa akidai kupingwa ukeketaji unahujumu tamaduni ya baadhi za jamii. Aidha anasema wanawake wote walio na miaka 18 na zaidi wanapaswa kuruhusiwa kuamua iwapo watapitia ukeketaji au la, bila kuzuiwa na sheria.

Ombi lake limepokea pingamizi kutoka wanaharakati wa kupinga ukeketaji, viongozi wa akina mama miongoni mwa mashirika mengine.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.