HabariMilele FmSwahili

Mahakama ya Kirinyaga kuamua kesi ya kupinga ushindi wa gavana Waiguru leo

Mahakama kuu ya Kirinyaga itatoa uamuzi leo kwa kesi iliyowsilishwa na kiongozi wa NARC Kenya kupinga ushindi wa gavana Anne Waiguru katika uchaguzi mkuu mwaka jana. Karua anaitaka mahakama kutupilia mbali matokeo ya uchaguzi huo akidai gavana Waiguru alishawishi matokeo ya ucaguzi huo. Kati ya mengine Karua anasema Waiguri alishirikiana na maafisa wa IEBC kufungia nje mawakala wake na kuwa tume hiyo ilifeli kuandaa uchaguzi huru na wa kuaminika. Hata hivyo gavana Waiguru kupitia wakili Paul Nyamodi ameyataja madai ya karua kuwa uvumi na kuwa hakuna ushahidi wa kudhibitisha kuwa uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu. Jaji Lucy Gitari atatoa uamuzi wake asubuhi hii.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.