HabariMilele FmSwahili

Waziri wa fedha Henry Rotich kusoma bajeti ya mwaka wa kifedha 2018/19 leo

Waziri wa fedha Henry Rotich leo atasoma bajeti ya shilingi trilioni tatu nukta sufuri saba kwa ajili ya matumizi ya mwaka wa kifedha 2018/19. Hata hivyo huenda serikali ikalazimika kukopa shilingi bilioni 562.74 kufadhili bajeti hii kutokana na upunugufu katika ukusanyaji wa mapato ya taifa. Hatua hii ikitarajiwa kuongeza kiwango cha madeni kufikia zaidi ya trilioni nne ya sasa. Katika bajeti ya mwaka huu serikali kuu itakabidhiwa mgao wa shilingi trilioni 1.6, idara ya mahakama shilingi bilioni 17.7 huku serikali za kaunti zikitengewa shilingi bilioni 372.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.