HabariMilele FmSwahili

Sukari iliyonaswa Eastleigh yapatikana na madini hatari kwa matumizi ya binadamu

Kuna hofu ya kuwepo katika baadhi ya duka za humu nchini sukari ilio na sumu ya madini ambayo ni hatari kwa matumizi ya binadamu. Waziri wa usalama Dr. Fred Matiang’ anasema uchunguzi uliofanyiwa sukari ilionaswa mtaani Eastleigh Nairobi umeashiria sukari hiyo ina madini ya Zebaki ama ukipenda Mercury. Matiang’ amelezea kusikitishwa na jinsi matapeli wanavyoleta nchini bidhaa gushi na kuhatarisha maisha ya wakenya.

Matiang’ amewataka wanaojihusisha na biashara hiyo kujisalimisha kwa polisi lau sivyo watakamatwa kwa lazima.

Amewaonya maafisa wa KRA,KPA na KEBS wanaoshirikiana na walaghai watakabiliwa kisheria.

Usemi wake umekaririwa na naibu mkuu wa utumishi wa umma Wanyama Musyambo

Show More

Related Articles