HabariMilele FmSwahili

DPP Noordin Haji akosoa EACC kwa uchunguzi duni dhidi ya kesi za ufisadi

Mkurugenzi wa mashataka ya umma Noordin Haji sasa anaikosoa tume ya ufisadi kwa uchunguzi duni dhidi ya kesi za ufisadi. Haji anasema uchunguzi huo hafifu umechangia kesi kadhaa kutupiliwa mbali na kwamba kuna haja ya EACC kuongeza kasi katika utendkazi wake. Akifika mbele ya kamati ya seneti kuhusu sheria, Haji ametoa mfano wa faili nne za ufisadi kuhusu magavana zilizowasilishwa kwake na EACC akisema baada ya kuzikagua alibaini ni kesi moja tu ina uzito
Akifika mbele ya kamati ya seneti kuhusu sheria Haji anasema hayuko katika shinikizo zozote kuwakabili watu fisadi.
Kadhalika,anasema wameweza kuwashtaki washukiwa wa sakata ya NYS kwa haraka kutokana na kuimarishwa ushirikiano baina ya idara za uchunguzi kinyume na ilivyokua awali.

Show More

Related Articles