HabariMilele FmSwahili

Zoezi la kuwachunguza maafisa wa uagizaji na ununuzi serikalini kuendelea

Zoezi la kuwachunguza maafisa wa vitengo vya uagizaji na ununuzi katika idara za serikali litaendelea. Ni baada ya jaji Onesmus Makau kutupilia mbali kesi iliowasilishwa na mwanaharakati Okiya Omtata kupinga uchunguzi huo. Katika uamuzi wake,Jaji Makau amesema madai ya Omtata kwamba uamzui huo ulikiuka sheria si kweli na kwamba hakuweza kushibitisha hilo. Jaji Makau amewapa maafisa hao siku 10 kuondoka afisini ili zoezi hilo kuanza mara moja. Rais Uhuru Kenyatta aliagiza maafisa hao kujiondoa afisini kwa mwezi mmoja kuchunguzwa walivyopata mali yao kufuata sakata za ufisadi zinazokumba idara tofauti za serikali wakati huu.

Akizungumza baada ya uamuzi huo,wakili mkuu wa serikali Ken Ogeto anasema zoezi hilo litaendeshwa kwa njia ya uwazi na kuzingatia sheria. Ameongeza hakuna anayelengwa moja kwa moja na kwamba watapokea mishahara yao kama kawaida na kupewa heshima hitajika.

Show More

Related Articles